Saidi Juma maarufu kama Chege Chigunda Mtoto wa Mama Saidi kutoka TMK ameumizwa sana na Msiba wa mwenzake Yessaya Ambilikile Y.P na Kuyasema haya...
"Innalilahi wa inna ilaih rajiun,sikuwahi kufikiria itatokea siku usiwe karibu yangu nilipigania sana uwepo wako katika kundi letu,wewe ndio ilikua remot yangu ktk uimbaji machozi yananitoka kila dakika nakumbuka mengi naujua msaada wako kwangu,tulipendwa sana kwa sauti zetu kufanana my brother,mungu ndio anajua kwanini ulipojitoa kundini nilipigania mpk uongozi
ukakurudisha,umeniacha ktk Hali ngumu sana na kuiacha Tmk wanaume family ktk majonzi makubwa yasio weza kufutika kirahisi hatuna la kufanya tena kwa sasa tunachofanya nikubaki tunakuombea kwa mwenyezi mungu akupunguzie adhabu na kukuweka mahala pema peponi RIP YP”
Msanii 'YP' toka kundi la TMK Wanaume Family ambaye alfariki jana usiku katika hospitali ya TEMEKE ambako alikuwa akisumbiliwa na kifua kwa muda mrefu lakini hali ilikuwa mbaya katika wiki mbili kabla ya kifo chake.
Meneja wa TMK Wanaume Family Said Fela amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Msiba wa msanii huyo uko Keko nyumbani kwa baba yake.
Said Fella amesema Marehemu ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambikile alifanya vizuri na msanii mwingine Y Dash na nyimbo kama 'Ulipenda Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama 'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume family.

Comments
Post a Comment