Skip to main content

Posts

Showing posts from January 19, 2015

WANAFUNZI WARUSHIWA VITOA MACHOZI BAADA YA KUANDAMANA WAKIDAI KIWANJA CHA SHULE YAO KIMENYAKULIWA....soma zaidi hapa

Polisi  katika mji mkuu wa Nairobi hii leo wamewafyetulia gesi ya kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchezea na mmiliki binafsi. Polisi hao wakiwa na Mbwa waliwatawanya wanafunzi hao, baadhi yao wakisemekana kuwa watoto wenye umri wa miaka sita baada ya kuuangusha ukuta mpya uliojengwa kati ya shule yao na uwanja huo. Wanafunzi hao walikuwa wamerejea shuleni Lang'ata baada ya mgomo wa wiki mbili wa walimu wa shule za umma walipopata kiwanja chao kikiwa kimeuzwa na hata kuwekwa uzio. Shule hio ina karibu wanafunzi 1,000 walio kati ya umri wa miaka mitatu na kumi na minne na inasimamiwa na baraza la jiji la Nairobi. Baraza la jiji limesema kuwa ardhi hio ni ardhi ya serikali ingawa halijazungumzia ambavyo ardhi yenyewe iliuzwa ingawa wanaharakati wanasema kiwanja hicho kimeuzwa kwa tajiri anayepanga kukitumia kwa ujenzi. Hizi ni baadhi ya picha za tukio hilo.