Msanii kutoka lebo ya WCB, inayoongozwa na DIAMOND PLATNUMZ , RAYVANNY amefunguka kuhusina na tetesi kwamba yeye ana kiburi na maringo kama wanavyosema baadhi ya watu. Rayvan amedaikuwa muda mwengine sheria na kanuni za kazi watu humuona mwenye maringo na kiburi kingi ambapo amedai ni kitu ambacho hawezi kuwanacho na hana. “Kwa mfano, ninaweza nikawa misingi yangu ya kazi inaniambia baada ya show inabidi niingie kwenye gari niwahi hoteli. Shabiki anataka nishuke, nipige picha, aniombe namba ya simu,” Ray alisema hayo kupitia kituo cha Kings FM nchini Tanzania. Anasema hayo ndio maagizo anayopewa na uongozi na ni lazima afuate maana ni muhimu sana katika maisha yake. “Huo ni msingi wa kazi, mtu hawezi kusema nimemdharau. Sometimes msingi wa kazi unaniambia haitakiwi nipokee simu ya interview ama simu ya promota akitaka show, anatakiwa apokee meneja, nitakavyomwambia ongea na meneja mtu ataona namdharau, lakini mimi nafuata msingi wa kazi, at end of the day siwezi ku...