Katika kundi la WASOJALIBAND wako vijana wanne ambapo mmoja ni ABILITY TOUCH , KHAMSO WASOJALI , IDRISS MOMBASANI pamoja na JAY BRO. Hapo jana walikua wanaenda kupiga show yao ya kwanza katika kaunti ya Tana River waliweza kuondoga Mombasa asubuhi kabisa ili kufika mapema wapumzike ndipo wapige show yao na warudi nyumbani Mombasa,Vijana hao waliweza kusafiri salama tena kwa ustaarabu mkubwa zaidi ila walipofika maeneo ya GARSEN ndio waingie HOLA kizaa zaa ndipo kilianza,kulingana na ripoti aliyoitoa manager wao ATHMAN BABAZ inasemekana waliweza kushukishwa wote na gari kuangaliwa kwaajili ya usalama zaidi. Kuanzia Kushoto : Khamso na Ability Vijana hao waliweza kuambiwa washuke kila mtu akiwa na kitambulisho chake mkononi hapo ndipo shida zilianza kwani wote wanne wanavyo vitambulisho ila ABILITY TOUCH kwasababu ya kuharakisha safari yeye alijipata amesahau Passport yake nyumbani,Askari hao hapo ndipo walipopata weak point na kumtia kijana huyo mbaroni kulingana na t...