Skip to main content

Posts

Showing posts from October 30, 2015

MTU WANGU NIMEKUSOGEZEA KIONJO CHA VIDEO MPYA YA CASH ERA INAYOTAMBULIKA KAMA "DEBORAH" PATA KUITIZAMA HAPA....

Cash Era ama ukipenda Mr.Chiringono amerudi tena katika kioo chako ambapo amekuja na kitu kipya kinachojulikana kama " DEBORAH ". THEGREATMULLEY imekua kipao mbele kukuletea taarifa mbali mbali na leo katika mitandao tumekumbana na kipande hichi cha sekunde arubaini cha video mpya ya CASH ERA inayojulikana kama DEBORAH Video yenyewe kiukamilifu inatarajiwa kuachiliwa wiki ijayo ambapo ni tarehe tatu 03|112015 video hio imeandaliwa na BIG DREAMS ambayo iko chini ya director RICKY BEKKO . Hicho ndicho kionjo cha video hio pata kukitazama na pamoja utoe maoni yako....

DIAMOND NA MAFIKIZOLO KWENYE HEADLINES TENA NA MARA HII NI NOMA ZAIDI SOMA HAPA UJUE WANACHOKIFANYA DIAMOND PLATNUMZ AKIWA NA KUNDI LA MAFIKIZOLO...Soma hapa zaidi

Mwaka jana star kutoka hapa Africa aliyechukua tuzo la Best World Wide Act hivi majuzi alikuwa kwenye vichwa vya habari pamoja na kundi kutoka nchini Afrika Kusini linalo tambulika kama MAFIKIZOLO. Waliweza kutupia picha kadhaa wakiwa studio wanafanya kazi na hizo picha zilibaki kuwa gumzo na ghafla kunyamaza,mashabiki wa wakali hao hawakujua kilicho kua kinaendelea lakini mapema leo hii DIAMOND PLATNUMZ aliweza kutweet kilichokua kinaendelea Diamond alikuwa anamjibu shabiki mmoja kupitia mtandao huo wakijamii na kuweka wazi kwamba kazi yake na kikundi cha MAFIKIZOLO iko njiani na video watakua wanaiandaa mwezi ujao. Kama wewe ni shabiki wa DIAMOND PLATNUMZ pamoja na MAFIKIZOLO vuta kita kaa mkao wakula mzigo utakua unaachiwa hivi karibuni..