. Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini nakuanza kumcharaza viboko kiongozi wa upinzani Bw. Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine. Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake na kuanza kucheza densi za kitamaduni kuwatumbuiza wageni pamoja na gavana wa jimbo hilo la Kwale Bwana Salim Mvurya katika mkutano wa kisiasa. Kiongozi huyo wa CORD alikuwa ameongozana na viongozi wengine kama sineta JUMA BOY,AGNES ZANI,JAMES ORENGO,JOHNSTONE MUDHAMA na wengine. Mwanamume huyo aliweza kumshambulia ODINGA ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana SALIM MVURYA ambaye ni gavana wa Jimbo hilo pia na kumchapa mara mbili.Hata hivyo mwanaume huyo alishindwa nguvu pale alipokabiliwa vikali na walinzi wa RAILA ODINGA . Polisi walithibitisha kuwa wamemkamata na kumwachilia baada yakugundua alikuwa na matatizo ya akili. Bado haijajulikana ni kwanini mwanamume huyo aliweza kumshambulia R...