Skip to main content

Posts

Showing posts from June 22, 2016

NEW GOSPEL VIDEO ALERT| WILLY PAUL NA BAHATI TUPA KULE PATANA NA EMJOMBA NDANI YA BINTI MCHUNGAJI

Kila kukicha kunazinduka talanta mpya katika tasnia ya muziki hapa Africa Mashariki na vijana wanaochipuka ni wenyewe sauti nzuri hata kuliko waliotangulia kama WILLY PAUL na BAHATI. Katika pitepite zetu ndani ya mitandao ya kijamii tuliweza kukutana na kichupa kipya cha msanii EMMANUEL MBAGI ama ukipenda EMJOMBA anayekuja vizuri katika gospel industry na video yake mpya inayojulikana kama BINTI MCHUNGAJI . Nyimbo hio imeweza kutengenezwa na produza mmoja anayejulikana kama RICHY BITZ ndani ya studio inayojulikana kama BITZ HOUSE MUSIC lakini kwasasa msanii huyo kwasasa yuko chini ya ALKA PRODUCTION STUDIOS AFRICA ambapo lebo hio ikiwa chini ya VEKTA KENYA ALKA imewahi kufanya kazi na wasanii wakubwa kama DNA , BIGPIN na wengine wengi na kwasasa inatafuta wasanii ili kufanya kazi nayo. Hii ndio video mpya msanii EMJOMBA ambayo imeweza kuketiwa chini na director kutoka Nairobi kwajina STEVE HUNTER