SABINA MKENYA ALIYE KUWA KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER ATIMULIWA NJE YA JUMBA HILO...soma sababu za kutimuliwa kwa mwanadada huyo hapa
Baada tu ya wiki mbili katika nyumba ya Big Brother Mwakilishi mmoja kutoka hapa Kenya Sabina ametimuliwa. Inasemekana kuwa Sabina ana mtoto wa miezi minane na ndio mkenya wa kwanza kutimuliwa kutoka katika nyumba hiyo. Inadaiwa kuwa watazamaji na mashabiki wa makala hayo waliamua kumuondoa Sabina baada ya siku 14 pekee ili aende kumuhudumia mwanawe. Sabina alionekana kumkosa sana mwanawe na wakati mwingi alionekana akifunga vitu kwenye mgongo wake ungedhani anambeba mtoto. Aliweka pamoja blanketi na nguo na kuvifunga kwenye mgongo wake akiwa na kofia ya mwanawe huku akitembea katika nyumba hiyo kabla ya kujiunga na wenzake waliokuwa wakijivinjari nje. Baadhi wanasema kufunga vitu mgongoni ndio chanzo cha mashabiki kuanza kuomuonea huruma Sabina wakisema bora aende nyumbani kwa mwanawe mwenye miezi minane. Na hapo ndipo walipompigia kura Jumapili na kumtimua kutoka Big Brother house. Sabina alitimuliwa kutoka katika nyumba hiyo pamoja na Lili...