Habari ya kusikitisha kwa mashabiki wa shindano la Big Brother Africa, Jumba linalotumika kufanyia shindano hilo lililoko Johannesburg, Afrika Kusini limeteketea kwa moto September 2. Kutokana na tukio hilo, M-Net na Endemol South Africa wameeleza kuwa wamelazimika kubadili ratiba ya shindano hilo msimu huu lililopewa jina la ‘ Big Brother Hotshots’ na halitaanza Jumapili, September 7 kama ilivyotarajiwa hapo awali. Chanzo cha moto huo hadi sasa hakijajulikana na makampuni hayo yameeleza kuwa uchunguzi wa kina utaanza mara moja. Makampuni hayo yamepata changamoto kubwa kutokana na tatizo hilo kwa kuwa vifaa vinavyotumika kufanyia uzalishaji ni vya aghali na adimu sana hivyo wameeleza kuwa ni vigumu kupata vifaa mbadala hivi punde. “Kila juhudi itafanywa kutafuta ufumbuzi wa tatizo haraka iwezekanavyo kuhakikisha kuwa reality show hii kubwa zaidi Afrika inaendelea.” Wameeleza katika tamko lao. Hakuna mtu aliyejuruhiwa katika tukio hilo. Haya ni maelezo wa...