Skip to main content

Posts

Showing posts from December 2, 2014

EXCLUSIVE VIDEO| RABBIT KING KAKA-LETA| WATCH IT HERE...

Baada ya kuachia wimbo wake  na video ya KICHINJIO msanii KAKA SUNGURA amerudi tena a na ujio mpya ambapo ameuachia hii leo wa video yake mpya inayojulikana kama LETA. Pata kuitizama video hio hapa..

KUNDI LA AL-SHABAAB LAKIRI KUHUSIKA NA MAUAJI YA WAKENYA 36....soma hapa zaidi

Kundi la wanamgambo nchini Somalia Al Shabaab limekiri kuwaua watu 36 katika shambulio lililotokea kwenye machimbo ya kokoto karibu na mji wa Mandera kaskazini mwa Kenya. Katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kundi hilo, wanamgambo hao wamesisitiza kuwa ndio waliowaua wakenya hao kwa sababu ya majeshi ya Kenya kuendelea kuwa nchini Somalia. Taarifa za mauaji hayo zilitolewa kwa mara ya kwanza na Shirika la Msalaba Mwekundu. Wakazi wa eneo hilo wamesema waathirika wote wa tukio hilo ni watu wasio Waislam ambao walikuwa wakifanya kazi katika machimbo hayo yaliyopo Kormey kilomita 15 kutoka mji wa Mandera Kaskazini mwa Kenya. Tukio hili linafuatia tukio la wiki moja iliyopita ambapo watu wapatao 28 waliuawa katika shambulio la basi la abiria huko Mandera. Kundi la wapiganaji wa Kiislam la Al Shabab limekiri kuhusika na mauaji hayo. Mkuu wa Polisi hilo amesema bado wanafuatilia tukio hilo. Katika tukio lingine, mtu mmoja ameripotiwa kuuawa nchini kufua