Skip to main content

Posts

Showing posts from November 17, 2014

NYOTA NDOGO ACHUKIZWA NA KITENDO CHA KUVULIWA NGUO KWA WANAWAKE OVYO OVYO.......soma alicho kisema hapa.

Huku maandamano ya wanawake yakiendelea katika miji mbali mbali nchini Kenya kwasababu ya wanawake kuvuliwa nguo msanii kutoka hapa Kenya Nyota Ndogo amekishutumu kitendo hicho na kudai kuwa pia wanaume wanao vaa surua milegezo wavuliwe pia. Mapema hii leo msanii huyo ameonekana katika mtandao wa Twitter akitupia maneno ya uchungu kufuatia kitendo haya ndio baadhi ya maneno... 1." KILA SIKU WEWE NDIO MUAMUZI WA MAISHA YAKO.MENGINE MUACHIE MWENYEZI MUNGU.UKITAKA KUVUTA BANGI PIA YANAMAISHA YAKE.MUAMUZI NI WEWE" 2." Bora kumpiga makofi mawali kama ilikua lazima kumuadhibu kwakuvaa nguo fupi.lakini sio kumvua nguo hadharani." 3." WANAUME WANAO VAA MA JEANS YAKUBANA PIA WAVULIWE.WANAO VAA NGUO ZINAZOITWA MUHARISHO YANI MATAKO NJE PIA WAVULIWE.ETI SWAGA SWAGA GANI.VUA"

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO MPYA WA MSANII MEDA UNAOJULIKANA KAMA "BARUA KWA DIAMOND"..Upate hapa

Wimbo huo unaojulikana kama BARUA KWA DIAMOND ni wa msanii kutoka Bongo/Tz alioamua kumwandikia Diamond ujumbe upate hapa chini..

WANAWAKE WAPINGA KUVULIWA NGUO OVYO OVYO NA WANAUME NCHINI KENYA....soma hapa na utizame picha za maandamano hayo.

Wanawake hapa nchini Kenya mapema hii leo wameandamana kupinga kitendo cha mwanamke mmoja kuvuliwa nguo wiki jana kwa madai kuwa alikuwa amevalia sketi fupi sana. Wanawake wengi walikerwa na kitendo hicho wakisema kuwa kila mwanamke ana haki ya kuvalia mavazi yanayomfurahisha. Hiyo wiki jana kanda ya video ilisambazwa kwa mitandao ya kijamii ikionyesha mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina hadi sasa akivuliwa nguo zake na wanaume katika kituo cha magari ya abiria kati kati mwa jiji la Nairobi. Wanawake mashuhuri wakiwemo wasanii, wanasiasa na wanaharakati walilaani kitendo hicho wakihoji kwani mavazi ya mwanamke yanamhusu nini mwanamume ambaye sio mumewe wala jamaa yake. Baadhi walikitaja kitendo hicho kuwa cha kinyama na kinachokiuka haki za wanawake. Msanii mmoja mashuhuri Nyota Ndogo alinukuliwa akisema ikiwa wanaume wanawavua nguo wanawake kwa kile wanachosema ni mavazi yasiyo ya kiheshima, basi na wanaume wanaolegeza long'i zao na wao basi pia wavul