Skip to main content

Posts

Showing posts from April 30, 2016

EXCLUSIVE STORY/MR.EXCLUSIVE|JE WAJUA WASOJALIBAND WALIKUA WAKITUMIA MIHADARATI? SKIZA HAPA LIVE MENEJA WAO ATHMAN BABA AKIFUNGUKA.

Ni kikundi cha wasanii wanne ambao wameweza kushika tasnia ya mziki kwa haraka sana kupitia ukakamavu wao pamoja na management yao. Kwa kuwatizama utasema kwamba ni vijana ambao wamelelewa katika mahandhari mazuri na yakufana lakini usilolijua ni kiza tena cha usiku wa manene, THE GREAT MULLEY MEDIA iliweza kumtafuta meneja wao anayejulikana kama ATHMAN BABAZ na kufunguka mengi kuhusu vijana hao wa WASOJALI BAND . WASOJALIBAND ni vijana waliokuwa wanarandaranda mitaa ya Kisauni/Mwandoni katika jiji la Mombasa ambao walikua kama chokora na walipatana na kama wanavyosema wakale kwamba usikate tamaa kwasababu hjui kesho yako,vijana hawa waliweza kukutana na jamaa mkarimu na mwenyewe moyo wa nyama na kuwasaidia na kuwalisha kama vile anawatambua. Pata kuiskiza Interview nzima hapa ATHMAN BABAZ akifunguka

KAMA ULIKOSA HAPO JANA NDANI BOXING LOUNGE PICHA NDIO HIZI HAPA NA VIDEO YA LE"GENERAL DEFAO AKIONGELEA KIFO CHA PAPA WEMBA..

Hapo jana ndani ya ukumbi wa BOXING LOUNGE mashabiki waliweza kuchezeshwa rumba na mumbaji mkongwe kuto Jamhuri ya Kongo LE'GENERAL DEFAO. Mziki huu wa wakubwa uliweza kuongozwa na RICKY MULOLO mwenyewe hit maker wa MZIZI pamoja na band yake nzima ,mbali na kusherekea huko na kucheza bila jasho LE'GENERAL DEFAO aliweza kuongelea swala zima la marehemu PAPA WEMBA "Kiukweli kama kuna muimbaji niliyekuwa na muheshimu kuliko wote ni marehemu PAPA WEMBA na yeye ndiye aliyenifanya hadi niingilie mziki maana nyimbo zake nilikua nazipenda sana na alikua akinipa moyo sana niliposikia kifo chake kiukweli niliumia sana na sikuamini hadi sasa naona ni kama vile bado niko ndotoni" Alisema Le'General. Pata kuzitazama picha na video hio isiozidi dakika mbili ya Defao akiongelea swala zima la yeye na marehemu. Hii hapa video pata kuitazama hapa