Skip to main content

Posts

Showing posts from July 26, 2016

NEW VIDEO ALERT| RAWBEENA-NIPOZE| HII NI NYENGINE KUTOKA KWA RAWBEENA ..Ipate hapa

Ni mmoja ya wanadada shupavu zaidi kimziki kutoka hapa Kenya ambapo mapema hapo jana aliweza kudondosha nyimbo yake mpya baada ya KITABU. Rawbeena ni msanii wakike kutoka hapa Kenya lakini katika kazi zake za usanii anazifanyia katika nchi jirani ya TANZANIA ambapo ana rekodi nyimbo zake zote ndani ya studio za MAZUU kule bongo Tz Tanzania. Kwasasa yuko humu nchini ambapo ameachia kichupa chake kinachojulikana kama NIPOZE ,tukikumbuka ni juzi tu msanii huyu wakike aliachia nyimbo yake iliojulikana kama KITABU ,Swali ni je kwanini RAWBEENA anaachia nyimbo zake kila baada ya mwezi au ndio mtindo wake anauanzisha?, kwa mengi tegea THEGREATMULLEYMEDIA upate umbea huu wote. Tazama Nipoze Hapa..

UKIKUTANA NA HUYU BEATIFUL ONYINYE UTAMSAHAU HUDDAH,VERA SIDIKA PAMOJA NA CORAZON KWAMBOKA..

Katika maisha kila mwanadamu ana mbinu ana mtindo wake wakuvua samaki yaani wakuleta kitu mezani ili maisha yaendelee na kusonga mbele. Ni mmoja kati ya wale wanaoupenda na kuuheshimu mziki wa hapa nyumbani,anakwenda kwajina la LUCY GALALWA kutokea maeneo ya Magharibi ya Kenya na ni mzaliwa wa papa hapa nchini. Lucy Galalwa ambae kwa jina la mitani ama jina lakazi yake anajulikana kama ELPARAISO aliweza kuongea na THEGREATMULLEYMEDIA mapema wiki hii na kumwaga kilio chake kwamba yeye anapenda mziki sana lakini aliweza kugundua kwamba kipaji cha kuimba ama kutoa poet hajajaliwa kuimba basi alitudokezea kwamba yeye kwavile anaupenda mziki na hana kipaji cha uimbaji,basi hivyo ameweza kuingilia mziki kwa upande wa UHALAKI ( SOCIALITE ). Aliongezea nakusema kwamba yeye anajiamini zaidi ya kila mtu anavyofikiria na atafanya vizuri tu na anaamini kwamba ataweza kama walio tangulia wenzake kama vile VERA SIDIKA , CAROZAN KWAMBOKA pamoja na wengine wengi kutoka humu nchini,