JAFFARYZO A.K.A RYZLEEN AAMUA KUENUA KUPELEKA VIDEO ZA WASANII WA HAPA NYUMBANI KATIKA NYANJA ZENGINE TOFAUTI KUFANYA HAYA HAPA....
Ni mmoja kati ya wasanii wanaojituma sana ili kuhakikisha kazi zake za muziki au sanaa yake inakaa vizuri na pia ni msanii aliyejishindia tuzo ya msanii bora anayechipuka mwaka jana katika tuzo za COAST MUSIC AWARD. Kwasasa amekuja na hii nyengine ambapo ameweza kuagiza vyombo vya kisasa vya ku-shoot video na kwasasa mikononi mwake anamiliki Drone ya kisasa inayokwenda kwajina MAVIC PRO pamoja na Camera kubwa kubwa na Lights za 4k ambazo unaweza kuzitumia hadi mchana kweupe na ameweza kufungua production yake ya video inayokwenda kwajina ANOTHER LEVEL FILMS ambayo yeye ndio mmliki. Tukizungumza nae pia aliweza kusema kwamba kwasasa yeye yuko mbioni kuhakikisha video za wasanii zinatanashatika kwa umiliki wa vyombo anavyomiliki na ataweza kusaidia vipaji maana kunawengi walio na uwezo wa kuimba ila uwezo wa kupata kichupa ndio hawana atasimamia hilo pia japo kwa maelewano. Kwasasa Jaffaryzo anajiandaa kufanya video yake mpya ya MAPENZI KIDONDO aliyomshirikisha ...