Skip to main content

Posts

Showing posts from December 5, 2018

MTANGAZAJI WA KIPINDI CHA MWAKE MWAKE GATES MGENGE ASEMA ARSENAL WAKIFUNGA ATATEMBEA.........Soma hapa zaidi

Moja kwa moja kutoka kwa mmiliki wa kipindi cha Mwake Mwake Eric Mgenge almaarufu kama GATES MGENGE mapema leo hii ametoa kiapo chake dhidi ya dimba litakalo sakatwa hapo saa tano usiku  jioni dhidi ya Arsenal na Manchester United. Kupitia ukurasa wake wa Facebook wa Eric Mgenge mtangazaji huyo aliweza kuapa yakwamba kama club ya Arsenal itaweza kuifunga club yake ya Man U basi ataweza kutembea kuanzia barabara za Lights hadi Mombasa mjini uku akipiga makelele Ya serikali Saidia " Leo Arsenal wakiwin pale kwetu home .....will walk from lights to town shouting ...serikali ..saidia saidia saidia." Tukirudi nyuma kiasi mtangazaji huyu pia aliweza kutoa kiapo chake kwa timu hizi hizi mbili na aliweza kuapa kutembea kwa miguu kuanzia Bamburi mwisho mpaka Bamburi mtambo kwa miguu na kipindi hicho aliweza kupata  bahati mbaya zaidi maana kulikua kunanyesha mvua kinoma noma. Sasa wacha kesho tuone kama ataliweza ili jua la Mombasa Kama akishindwa.