Skip to main content

Posts

Showing posts from August 25, 2016

EXCLUSIVE STORY|LEBO YA WCB KUMSAINI MSANII MWENGINE WA R&B ANAYETOKA PANDE ZA MOROGORO JE NI NANI PATA KUMJUA HAPA.......

Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii wa muziki wa R&B ,Belle 9 na yeye akasaini ndani ya label hiyo. Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘ Bugger Movie Selfie ’ ameonekana akifanya mazoezi ya bendi ya Diamond katika ofisi za WCB. Kwa mujibu wa FB ya EATV, Belle pamoja na Diamond wameonekana wakiimba wimbo ‘ Mdogo Mdogo ’ kwa pamoja huku wakicheza. Hatua hiyo imefufua matumaini mapya kwa mashabiki wa kumuziki kuona huweza WCB ikamsaini msanii huyo kama ilivyofanya kwa Rich Mavoko. Kwa sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka Rayvany pamoja Queen Darlin.

WASANII KUTOKA AFRIKA MASHARIKI KUPATA SABABU YA KUTABASAMU HII BAADA YA TRACE TV KUFUNGUA KITUO KIPYA CHA TRACE MZIKI

Kituo cha televisheni cha TRACETV kinachoaminika kupeperusha nyimbo mpya na kali kutoka Afrika pamoja na Uingereza. TRACETV Mwezi ujao watakua wanazindua kituo kipya kinachokwenda kwajina TRACE MZIKI ambacho kitakua kinacheza asilimia { 100% } mziki wa kutoka Hapa Africa Mashariki. Nchi zitakazo nufaika na kituo hicho ni KENYA,UGANDA,TANZANIA,RWANDA,BURUNDI ambapo kitakua kinazindua video mpya za wasanii kutoka Afrika MAshariki, Mbali na TRACE MZIKI pia watakuwa wanazindua vituo vyengine viwili ambapo ni TRACE NAIJA pamoja na TRACE AFRICA kumbuka kitakua kianaaznza kupeperusha ratiba zake tarehe moja mwezi ujao yaani 1|09|2016.