Wikendi hii ilikua ni ndefu ya siku kumi za burudani ambapo kulikuwa na tamasha la MOMBASA INTERNATIONAL CULTURAL ambapo liliweza kutamatika hapo jana katika uwanja wa MAMANGINA. Kati ya wasanii waliopiga show hio ni SUSUMILA,DAZLAH,AMOURY BEYBY pamoja na bongo finest ALLY KIBA,Kati ya hao kikundi cha vijana wanne wanaokuja katika game kwa kasi WASOJALI band inasemekana hawakupewa nafasi nzuri juu ya stage kufanya mambo yao. AMOURY BEYBY akiwa jukwaani. Katika ukurasa wa facebook wa WASOJALI BAND waliweza kuandika maneno haya " Mombasa international Cultural festival hawakutupa uhuru wa kuperform kwa stage kabisa hatukufurahia show ya festiva l" Yakiambatanishwa na picha wakiwa juu ya jukwaa,tukiongea na manager wa vijana hao anayetambulika kama ATHMAN BABZ alisema "Vijana walikuwa wamejipanga vizuri na show hio lakini muda waliopewa juu ya jukwaa haukunifurahisha kabisa kwani walipelkwa mbio ni kama walikua vitani" Alisema hayo Meneja Athman Babaz....