Sudi Mohamed Sudi ambaye kwasasa anatamba na hit yake mpya inayokwenda kwajina KIDONDA kwasasa yuku jijini Mombasa anaifanyia nyimbo hio media tour za upande wa Pwani. Hapo jana SUDIBOY aliweza kuzuru maeneo yalioathirika na baa la njaa maeneo ya KASHANI katika wodi ya Bamburi Kiemebeni pale alipopeleka msaada kwa mayatima pamojana wajane. Msanii huyo aliweza kuandamana na wasanii wenzake kama KIGOTO pamoja na crew yake nzima ya SUDI WEZESHA,tukiongea nae hapo jana aliweza kutudokezea kwamba ameweza kuanzisha msingi wake mpya utakao kuwa unasidia WAJANE,MAYATIMA pamoja na MASIKINI wasio jiweza katika jamii yetu. Baada ya Mzazi kuanzisha foundation yake inayojulikana kama MZAZI FOUNDATION kutoka Pwani ya Kenya SUDIBOY ni msanii wakwanza kufuata mkondo huo wakuwezesha jamii kuishi vizuri na kile atakacho pata kidogo agawane na wenzake wasio jiweza. Hizi ndio baadhi ya picha akiwa na Wajane pamoja na mayatima akiwapa msaada wa vyakula pamoja na viwalo. ...