Msanii OHZY ukipenda T.U (Tayari Ushajua) aliweza kueka sakata la muziki kando ili kuwajibika na mambo yake ya kijamii pamoja na kumtunza mke wake beautiful Onyinye wake. Katika show kubwa ya BlazeKenya iliofanyika weekendi iliopita msanii huyo alionekana akiwa na mwenzake ambaye alikua ni DAZ EX akiwa ametoboa kipuli cha pua yaani KIDANI cha pua,mbali na hapo pia katika ukurasa wake wa Faceboo na Instagram aliweza kushare picha akiwa na Daz Ex kipuli kikionekana uku akiweka Caption ya " CHUMA KWENYE PUA " swali ni jee ameacha mziki na kuingilia ubishow? Katika maojiano yetu naye msanii huyo wa kundi la X-MATHARE aliweza kusema kwamba kutoboa pua ni mapambo tu na sio ati ana maana nyengine na ameamua kutoboa pua kwasababu ni mapenzi yake na amependa yeye mwenyewe "Sio ati nimetoboa pua kwakuiga watu la! nimetoboa kwa mapenzi yangu na hakuna aliyenishawishi ila mimi mwenyewe na nafsi yangu na pia nashkuru mama watoto wangu swala hili hajalibeba kiuzito na pia ame...