Msanii kutoka Mombasa/Kenya Benso ambaye pia aliweza kushinda tuzo ya mwana muziki bora wa kiume katika tuzo za mwaka jana katika COAST MUSIC AWARDS hii leo amefunguka kuhusiana na video yake alioachia mapema wiki hii. Tuliweza kukutana na BENSO na tukaweza kumuulia maswali kadhaa kuhusiana na karia yake ya mziki msanii huyo aliweza kusema kuwa yeye katika jambo hujiamini ndio maana hufanya kazi zake kiuwakika bila kuangalia na amefanya nini ama nini kinachoendelea katika mziki. Tuliweza kumuuliza video aliyoitoa imemgharimu pesa ngapi ama kiwango gani cha pesa haya ndio aliyasema " Kiukweli siwezi sema video ni pesa ngapi lakini kiukweli imenigharimu na me hupenda ni gharamike ili mafans wangu na familia yangu ya mashabiki wawezekuona kazi nzuri na ni navyo jituma kimziki" Alisema. Benso aliweza pia kufunguka kuwa video hio yake mpya kwa jina IMEREMENDE kuna sehemu aliitajika kuingia ndani ya BOMAS OF KENYA alioko jijini Nairobi ivo aliweza kuenda na...