Skip to main content

Posts

Showing posts from October 22, 2018

BABU TALE ATOA RIPOTI YA VILE KUNAVYOENDELEA INDIA BAADA YAKUMPELEKA "HAWAA" KWA MATIBABU

Khamisi Taletale kutoka kiwanda cha mziki cha WC.B almaarufu kama Babu Tale ambaye ndiye manager wa msannii DIAMOND PLATNUMZ ametoa taarifa fupi kumhusu msanii wakike HAWAA . Tunamkumbuka sote msanii wakike HAWAA aliyewahi kufanya hit song moja na Diamond Platnumz iliyojulikana kama NITAREJEA iliyogusa nyoyo na nafsi za watu wengi sana kutoka Africa Mashariki. Msanii Huyo wakike alipatikana na mtihani wakuwa ini lake lina matatizo na hivyo basi anahitaji upasuaji kwani afya yake haikua njema. Kupitia kurasa zake za Instagram Babu Tale aliweza kueka picha ya Hawa uku akitanguliza na maneno haya " Asante Mungu tumefika salama India na tumefanya vipimo vyote upya salama na jibu lililotoka kwa wataalamu kwa asilimia 95% awajaona tatizo linalohusiana na ini kwa mgonjwa ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini ivyo basi kutaitajika kufanyika upasuaji mkubwa ambao utakua na uangalizi mkubwa wa wataamu then wametuakikishia baada ya hapo mgonjwa atapata nafu