Hizi ni video tatu kali na mpya kutoka kanda ya Mombasa na utunzi uliosimama katika mashairi na director waliosimama katika kazi izo.. 1. Hii hapa ni moja ya kwanza kutoka kwa msanii wakike anayejulikana kama KENYAN FLAG LADY a.k.a VIVONCE WANDIA ambaye mwanadada huyu alikua amepiga kimya kwa muda mrefu hadi jamii yake ya mziki ilikua inaanza kukata tamaa naye,hivi sasa amerudi kivyengine na melody kali pamoja na utunzi uliosimama, nyimbo yake mpya aliyoitilia sauti katika studio za TEMPOZ chini ya produza AMZ WA LEO inajulikana kama RUDI KULE imeongozwa na director JOHNSON KYALO, video hio kwasasa inafanya vizuri ambapo ina siku tano tangu kuekwa katika ukurasa wa YOUTUBE na sasa imefika views elfu kumi na sita yaani ( 16,135 views) HII HAPA BONYEZA KUITIZAMA 2. Video inayoshika nambari yapili inakwenda kwajina MAJINI kutoka kwa msanii wa michano ama mwana-HIP-HOP ambaye pia alikua amepiga ukumya mwaka mmoja hapa namuongelea KAA LA MTO,na video yake kwasasa ime...