Skip to main content

VIDEO TATU KALI KUTOKA PWANI YA KENYA NA ZILIZOSIMAMA..HIZI HAPA....BONYEZA KUTIZAMA

Hizi ni video tatu kali na mpya kutoka kanda ya Mombasa na utunzi uliosimama katika mashairi na director waliosimama katika kazi izo..

1.
Hii hapa ni moja ya kwanza kutoka kwa msanii wakike anayejulikana kama KENYAN FLAG LADY a.k.a VIVONCE WANDIA ambaye mwanadada huyu alikua amepiga kimya kwa muda mrefu hadi jamii yake ya mziki ilikua inaanza kukata tamaa naye,hivi sasa amerudi kivyengine na melody kali pamoja na utunzi uliosimama,
nyimbo yake mpya aliyoitilia sauti katika studio za TEMPOZ chini ya produza AMZ WA LEO inajulikana kama RUDI KULE imeongozwa na director JOHNSON KYALO, video hio kwasasa inafanya vizuri ambapo ina siku tano tangu kuekwa katika ukurasa wa YOUTUBE na sasa imefika views elfu kumi na sita yaani (16,135 views)

HII HAPA BONYEZA KUITIZAMA
 2.
Video inayoshika nambari yapili inakwenda kwajina MAJINI kutoka kwa msanii wa michano ama mwana-HIP-HOP ambaye pia alikua amepiga ukumya mwaka mmoja hapa namuongelea KAA LA MTO,na video yake kwasasa imemrudisha na inafanya vizuri katika ukurasa wa YOUTUBE tukizingatia kwamba video hio imeweza kuelekezwa na director JOHNSON KYALO,nyimbo hio MAJINI imetoka katika mikono ya produza TENKIXX katika ukurasa wa Youtube imeweza kugonga views elfu nne yaani (4,191 views).

Hii hapa chini pata kuitizama.



3.
Video inayoshika nambari yatatu ni kutoka kwa hitmaker wa KIDE KIDE hapa namzungumzia DAZLAH KIDUCHE wimbo kwajina NAOMBA FURAHA, wimbo huu wake ameweza kuutengeneza katika studio za TEE HITS chini ya produza TEE TONY, video yake imeweza kuongozwa na director LAMAR ambapo huyu ni director anayekuja vizuri katika anga za uongozaji wa video,kichupa hiki kinafanya vizuri katika mtandao wa YOUTUBE ambapo kwasasa imefika watazamaji elfu tatu yaani (3,470 views).

PATA KUITAZAMA KWA KUBONYEZA LINK HAPA CHINI .

Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE HII HAPA : MASAUTI KATABIRIWA KUWA "THE NEXT BIG THING" NDANI YA MWAKA 2019 JE UNAJUA NI NANI ALIYEMTABIRIA?..Soma hapa

Katika miaka yote mwaka wa 2018 unaonekana ndio mwaka ambao mkali wa masauti Shembwana Masauti ameweza kufanya kazi nyingi nzuri na za ghali sana. Mkali wa 'vocals' Masauti mwaka jana aliweza kudondosha ngoma kali takriban kama nne kwa mfululizo amabazo ziliweza sana na kwasasa kibao kinachotatiza anga kinaitwa KIBOKO ambacho kibao icho kinaendelea kufanya vizuri ndani Afrika Mashariki. Hapo jana Presenter mkubwa kutoka MileleFmJalang'o almaarufu kama Mzee Jalas Mwenyewe aliweza  kusema msanii huyu huu mwaka ndiye atakaye sumbua kulingana na usimamizi wake mzuri pamoja na kazi zake zinazoweza kupita kiwango. Hii Hapa ndio kazi yake MAsauti mpya inayokwenda kwajina KIBOKO

EXCLUSIVE: DOWNLOAD WIMBO MPYA WA TANZANITE ALIYO MUIMBIA LULU WA BONGO MOVIE

Pata kudownload na kuskiza hapa chini....

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.