Wanasema kula cha ndugu si haramu,ndio maana msanii anayekuja kwa kasi katika tasnia ya Bongo Fleva Harmonize akaamua kutoka na Jacqueline Walper aliye kuwa mpenziwe DIAMOND PLATNUMZ. Inaonekana si tetesi tena kwasababu CEO wa WCB mwenyewe ametoa baraka zake kwa wawili hao, Harmonize na Jacqueline Wolper ambao yeye anawaita ‘love birds.’ Diamond na Wolper waliwahi kuwa na uhusiano miaka kadhaa iliyopita. Muimbaji huyo wa ‘Make Me Sing’ amepost video inayomuonesha Harmonize akiwa kwenye gari na mpenzi wake huyo mpya huku akimuimbia hit ya bosi wake, Number One. “A throw Back of two love Birdsbirdrevolving_hearts…. Mjini kutamu jamani… hebu nitagie Wakereketwa hapa, waje kuzirai….?” ameandika Diamond kwenye video hiyo. Naye dada yake, Esma hakusita kulipigia chapuo penzi hilo jipya kwa kuiweka video hiyo na kuandika: Karibu ktk familia yetu @wolperstylish mawifi tunagubu but utuzoee ila nawee usije kuwa na roho mbaya mjengoni mchaga wewe harmo wetu tumetoka nae m...