Skip to main content

Posts

Showing posts from March 31, 2017

EXCLUSIVE STORY||| NYOTA NDOGO AWATOA POVU WANAOTETA MBONA HAZEEKI

Staa wa kike wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Kenya maarufu kama Nyota Ndogo, amewajibu watu wanaoonekana kumfuatilia maisha yake binafsi. Nyota ambaye alizaliwa mwaka 1981, amekuwa kwa game ya muziki tangia mwaka wa 2004 ambapo tokea hapo amekuwa akitoa hits za muziki kila anapoingia studioni kurekodi. Muziki kwake umekuwa kila kitu, na si mara moja amekuwa akihoji kwenye vituo vya habari kuwa hata nyumba anayoishi kwa sasa imejengwa na pesa za muziki pamoja na biashara nyingine ambazo zinazidi kumtilia kipato cha kila siku. Nyota ni baadhi ya mastaa wa muziki wa nchini Kenya wanaoheshimika sana, na pia amekuwa katika mstari wa mbele katika wale mastaa wakongwe nchini Kenya ambao hawakosi show kila wakati. Hata hivyo mbali na mafanikio hayo, Nyota Ndogo katika maisha yake ya kawaida hakosi kupitia changamoto za kimaisha kama staa wengine Afrika. Leo kupitia ukurasa wake wa Facebook, Nyota ametupia ujumbe unaonekana kuwasuta watu fulani wenye kupenda k