Skip to main content

Posts

Showing posts from March 27, 2015

EXCLUSIVE VIDEO| WILLY PAUL MSAFI-VIGELEGELE| WATCH IT HERE...

Willy Paul Msafi baada ya kumpata mamake sasa ameachia video yake inayojulikana kama VIGELEGELE . Tukikumbuka msanii huyo wa nyimbo za injili mapema wiki hii alikua anamtafuta mamake mzazi aliyekuwa amepotea na ndipo msanii JAGUAR alichukua jukumu hilo la kumsaidia ili kumpata mamake na kwasasa msanii huyo anajihisi huru na kuachia wimbo wake. Mapema hii leo Willy ameachia ngoma yake mpya baada ya kimya cha nyimbo ya MAMANGU  sasa msanii huyo amekuja na njia nyengine na video hio ya VIGELEGELE. Pata kuitazama video hio hapa na uangushe comment yako.

EXCLUSIVE VIDEO| PATA KUITIZAMA VIDEO MPYA YA SHETTA AKIWA AMEMSHIRIKISHA K-CEE-SHIKOROBO....Itizame hapa

Baada ya kimya cha mda msanii kutoka nchini Tanzania hit maker wa KEREWA namzungumzia Shettah ameachia mzigo mwengine ambao unakwenda kwa jina SHIKOROBO. Round hii Shetta hakumshirikisha tena DIAMOND PLATNUMZ bali alirusha ndoana yake hadi maji marefu na kumnasa msanii wa nchini Nigeria anayejulikana kama K-CEE,wasanii hao walikutana na kutengeneza ngoma wakaiita SHIKOROBO ambapo waliitengeneza katika studio za TUDDY THOMAS nchini Tanzania. Video hio imeketiwa chini na Director kutoka SOUTH AFRICA kwa jina GODFATHER. Hii ndio Video ya Shikorobo itzime alafu angusha maoni yako hapo chini...