Skip to main content

Posts

Showing posts from January 22, 2015

WEMA SEPETU AMFUNGULIA DIAMOND PLATNUMZ KESI KWA KUDAI KUWA ANA DENI LAKE LA MILLIONI 10...soma hapa zaidi.

Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Wema Sepetu,amemfungulia kesi ya madai mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, kwa kumtapeli kiasi cha Sh milioni 10. Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la Utangazaji (BBC) idhaa ya Kiswahili, Wema aliripoti madai yake kituo cha Polisi Oysterbay akidai kuwa alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa makubaliano ya kazi na kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume makubaliano yao. Muhusika mkuu ambaye ni Wema alitoa maelezo kwamba watu wanamtupia lawama kutokana na hatua aliyofikia, lakini amedai kuwa amelazimika kufanya hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeingia dhamana na taasisi Focus Vicoba kuchukua fedha hizo. “Naona watu wengi wananilaumu kwa kuwa nimemfungulia kesi Diamond, pasipo kuelewa kama fedha hizo pia hazikua zangu bali ni mkopo ambao niliingia dhamana katika taasisi ya utoaji mikopo ya Vicoba. “Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili aweze kuand