Skip to main content

WEMA SEPETU AMFUNGULIA DIAMOND PLATNUMZ KESI KWA KUDAI KUWA ANA DENI LAKE LA MILLIONI 10...soma hapa zaidi.




Mwigizaji wa filamu nchini Tanzania Wema Sepetu,amemfungulia kesi ya madai mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’, kwa kumtapeli kiasi cha Sh milioni 10.

Kwa mujibu wa mtandao wa Shirika la Utangazaji (BBC) idhaa ya Kiswahili, Wema aliripoti madai yake kituo cha Polisi Oysterbay akidai kuwa alimpatia mwanamuziki huyo kiasi hicho kwa makubaliano ya kazi na kuahidi kumlipa, lakini amekwenda kinyume makubaliano yao.
Muhusika mkuu ambaye ni Wema alitoa maelezo kwamba watu wanamtupia lawama kutokana na hatua aliyofikia, lakini amedai kuwa amelazimika kufanya hivyo kwa kuwa yeye ndiye aliyeingia dhamana na taasisi Focus Vicoba kuchukua fedha hizo.
“Naona watu wengi wananilaumu kwa kuwa nimemfungulia kesi Diamond, pasipo kuelewa kama fedha hizo pia hazikua zangu bali ni mkopo ambao niliingia dhamana katika taasisi ya utoaji mikopo ya Vicoba.
“Kupitia mfuko wa Focus Vicoba nilichukua mkopo huo kwa lengo la kumpatia Diamond, ili aweze kuandaa miradi yake tena kwa makubaliano kuwa atazirudisha ili tuweze kufanya marejesho ya mkopo tuliochukua,” alisema Wema.
Mrembo huyo alieleza muda waliiopeana ahadi ya kurudisha fedha hizo umepita na Diamond haoneshi dalili ya kuzirejesha wakati wanatakiwa kuzirudisha kwa wakati .

“Yote haya yasingenikuta, lakini sina jinsi kwani natakiwa kurudisha pesa za watu nimekuwa nikimpigia simu Diamond hataki kupokea simu zangu, lakini kama alitaka kunidhulumu ni bora angejiunga mwenyewe na hawa Vicoba ili apate mkopo na kufanya mambo yake au kama aliona hawezi kwa kujishtukia basi angetumia ile tovuti yao, angepata kwa urahisi na hakuna mtu yeyote angejua kama amekopa ila sio kukimbia kulipa deni la watu,” alisema.
Wema ambae alimwekea dhamana, yupo katika kipindi kigumu ambacho kinaweza kupelekea kufilisiwa mali zake ambazo aliziandikisha wakati wa kuchukua mkopo huo ili ziweze kufidia deni hilo.
Kwa mujibu wa kiongozi wa taasisi hiyo ambae aligoma kutajwa jina lake gazetini, alisema kuwa ni kweli Wema alifika katika ofisi zao zilizopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, ili apewe muongozo lakini alipotakiwa kufuata taratibu za kiofisi kama wanachama wengine wanavyofanya katika vikundi, hakukubaliana na utaratibu, hivyo kushauriwa ajiunge kupitia tovuti .
Alipotafutwa  Meneja wa Wema, Martin Kadinda,  kuzungumzia swala hili  alisema hajui chochote kuhusu kufungulia kwa kesi hiyo, akaomba apewe muda kumtafuta msanii huyo ili aweze kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, lakini hakueleza nini kilichojiri na kusisitiza asubiriwe.
Pia  alipotafutwa meneja wa Diamond, Babu Tale, kuzungumzia swala hili  alionekana kushtushwa na habari hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania

Powered by BBC

Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.  

NEW SONG ALERT: NYOTA NDOGO-SUBIRA YANGU| IPAKUE HAPA...

Hii ni ngoma mpya ya msanii wakike NYOTA NDOGO inayokwenda kwajina SUBIRA YANGU ambapo ngoma hii aliweza kuiachia hapo jana. Pata kuipakua hapa ivi upate ujumbe mtamu na Wakuelimisha.

NEW AUDIO | RABBIT KING KAKA FEAT RICH MAVOKO-NJOO | LISTEN AND DOWNLOAD HERE..

Hii ni nyimbo mpya kutoka KenyaTanzania ambapo ni moja ya Colabo iliyongojewa kwa muda mrefu,colabo hio inakwenda kwa jina la NJOO ambapo ni msanii wa Hip Hop ameshirikisha msanii wa Bongo flava kutoka Tanzania hapa nikiwa namzungumzia KING KAKA akiwa na RICH MAVOKO. Nyimbo hio imeachiliwa rasmi hii leo na wasanii hao wawili. pata kuiskiza na ku download hapa..