SABINA MKENYA ALIYE KUWA KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER ATIMULIWA NJE YA JUMBA HILO...soma sababu za kutimuliwa kwa mwanadada huyo hapa
Inasemekana kuwa Sabina ana mtoto wa miezi minane na ndio mkenya wa kwanza kutimuliwa kutoka katika nyumba hiyo.
Inadaiwa kuwa watazamaji na mashabiki wa makala hayo waliamua kumuondoa Sabina baada ya siku 14 pekee ili aende kumuhudumia mwanawe.
Sabina alionekana kumkosa sana mwanawe na wakati mwingi alionekana akifunga vitu kwenye mgongo wake ungedhani anambeba mtoto.
Baadhi wanasema kufunga vitu mgongoni ndio chanzo cha mashabiki kuanza kuomuonea huruma Sabina wakisema bora aende nyumbani kwa mwanawe mwenye miezi minane.
Na hapo ndipo walipompigia kura Jumapili na kumtimua kutoka Big Brother house.
Sabina alitimuliwa kutoka katika nyumba hiyo pamoja na Lilian kutoka Nigeria na Esther wa Uganda.
Hatua ya kumondoa Sabina katika Big Brother house inamwacha mwakili mmoj tu wa Kenya Melvin Alusa ambaye ni kakake Ben aime Baraza wa kikundi cha wanamuziki cha Sauti Sol.
Comments
Post a Comment