Skip to main content

RAILA ODINGA ASHAMBULIWA KWA VIBOKO KATIKA COUNTY YA KWALE....Tazama video hio hapa...


.

Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini nakuanza kumcharaza viboko kiongozi wa upinzani Bw.Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.

Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake na kuanza kucheza densi za kitamaduni kuwatumbuiza wageni pamoja na gavana wa jimbo hilo la Kwale Bwana Salim Mvurya katika mkutano wa kisiasa.

File:Raila Amolo Odinga - World Economic Forum on Africa 2008 1.jpg
Kiongozi huyo wa CORD alikuwa ameongozana na viongozi wengine kama sineta JUMA BOY,AGNES ZANI,JAMES ORENGO,JOHNSTONE MUDHAMA na wengine.

Mwanamume huyo aliweza kumshambulia ODINGA ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana SALIM MVURYA ambaye ni gavana wa Jimbo hilo pia na kumchapa mara mbili.Hata hivyo mwanaume huyo alishindwa nguvu pale alipokabiliwa vikali na walinzi wa RAILA ODINGA.

Polisi walithibitisha kuwa wamemkamata na kumwachilia baada yakugundua alikuwa na matatizo ya akili.
Bado haijajulikana ni kwanini mwanamume huyo aliweza kumshambulia Raila ila baadhi wanasema mwanamume huyo alighadhabishwa pale waziri mkuu aliweza kucheza densi na mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wakinamama waliokuwa wanatumbuiza wageni waheshimiwa.


Unaweza kuitazama Video hio Hapa.

Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.  

NEW SONG ALERT: NYOTA NDOGO-SUBIRA YANGU| IPAKUE HAPA...

Hii ni ngoma mpya ya msanii wakike NYOTA NDOGO inayokwenda kwajina SUBIRA YANGU ambapo ngoma hii aliweza kuiachia hapo jana. Pata kuipakua hapa ivi upate ujumbe mtamu na Wakuelimisha.

NEW AUDIO | RABBIT KING KAKA FEAT RICH MAVOKO-NJOO | LISTEN AND DOWNLOAD HERE..

Hii ni nyimbo mpya kutoka KenyaTanzania ambapo ni moja ya Colabo iliyongojewa kwa muda mrefu,colabo hio inakwenda kwa jina la NJOO ambapo ni msanii wa Hip Hop ameshirikisha msanii wa Bongo flava kutoka Tanzania hapa nikiwa namzungumzia KING KAKA akiwa na RICH MAVOKO. Nyimbo hio imeachiliwa rasmi hii leo na wasanii hao wawili. pata kuiskiza na ku download hapa..