Skip to main content

MAMA NAY WA MITEGO AINGIWA NA WASIWASI KWA VIDEO ALIOITOA MWANAWE NAY.Soma hapa alicho kisema..




nay 5
Mama mzazi wa mkali wa bongofleva Nay wa Mitego ameongea kwa mara ya kwanza na millardayo.com na kusema ana wasiwasi na mwanae ambae hivi karibuni ametoa video mpya aliyoifanya nchini Kenya.
Amekiri kweli kwamba siku kadhaa zilizopita ilibidi amwite na kumuweka chini Nay wa Mitego akitaka amueleze kama ni kweli amejiunga na ‘freemason’ ambayo wengi wanaitafsiri kwamba ni dini ya kumwabudu shetani kitu ambacho kiliwahi kukanushwa na aliyewahi kuwa mmoja wa viongozi wa freemasons Tanzania.
Mama anasema alimketisha Nay chini baada ya video ya ‘Mr. Nay’ kutoka ambapo baadhi ya picha sio za kawaida mfano damu pamoja na alama zilizotumika ndani yake.
nay 4
 Amesema ‘Naitwa Matilda Mwaipopo ni mama mzazi wa Nay, kwakweli mwanangu namchukulia lakini sifa tu zinazokuja kama Nay kwenye magazeti, Nay freemason, watu wanakuja wananisimamisha…. mwanao Nay kweli? mbona tunasikia freemason? basi kichwa changu kinapagawa…. ‘
‘Nikiangalia miziki anayoifanya kama hii aliyoitoa juzi, jamani mwanangu anaambiwa freemason usikute kweli freemason, Nay wa Mitego nimemuita…. mwanangu vipi? ninayoambiwa ni ya kweli? Freemason wewe? mbona wimbo wako huu siuelewielewi?  ananiambia mama mimi sio freemason, namwambia hapana mwanangu hapana….. nasikia freemason watu wanatoaga hata wazazi sadaka’


 nay 3
‘Mimi ndio mama niliebakia baba yenu alifariki aliniacha ukiwa na miaka mitatu nimejitahidi kukulea mpaka leo…… unitoe sadaka mama yako kweli?????!!! Nay wa Mitego sana ni kucheka…… anaona tu mama kama anapagawa, lakini kwakweli mwanangu simuaminiamini miziki yake hii anayoifanya’






nay 2

 Nay 1
Source:Millard-Ayo




Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.  

NEW SONG ALERT: NYOTA NDOGO-SUBIRA YANGU| IPAKUE HAPA...

Hii ni ngoma mpya ya msanii wakike NYOTA NDOGO inayokwenda kwajina SUBIRA YANGU ambapo ngoma hii aliweza kuiachia hapo jana. Pata kuipakua hapa ivi upate ujumbe mtamu na Wakuelimisha.

NEW AUDIO | RABBIT KING KAKA FEAT RICH MAVOKO-NJOO | LISTEN AND DOWNLOAD HERE..

Hii ni nyimbo mpya kutoka KenyaTanzania ambapo ni moja ya Colabo iliyongojewa kwa muda mrefu,colabo hio inakwenda kwa jina la NJOO ambapo ni msanii wa Hip Hop ameshirikisha msanii wa Bongo flava kutoka Tanzania hapa nikiwa namzungumzia KING KAKA akiwa na RICH MAVOKO. Nyimbo hio imeachiliwa rasmi hii leo na wasanii hao wawili. pata kuiskiza na ku download hapa..