Skip to main content

MZOZO BAINA YA KAA LA MOTO KIUMBE NA JOHNY SKANNY WACHUKUA HATAMU NYENGINE.....Soma aalichokisema Kaa La Moto hapa..

Mzozo ulio ibuka wiki hii baada ya tamasha la STYLAS AWARDS kutamatika wiki mbili zilizopita,KAA LA MOTO KIUMBE alidai kuwa msanii mwenza wa HipHop anayejulikana kama JOHNY SKANY alimkaribisha kimadharau katika jukwaa la STYLAS kama msanii mchanga wa HipHop anayeibukia.

Baada ya hapo ilichukua hatamu nyengine pale walianza kutupiana katika mitandao ya kijamii maneno ya chuki na mizozano ambapo Kaa La Moto alidai kuwa msanii Skanny awachie wenzake jukwaa kwani yeye amechoka na niwakitambo jambo lilo muudhi msanii Skanny nakuandika "
Nakupa chance uonekane alafu unaleta kichwa!!!hahahahahah watoto wa leo balaa.tulia tukulee ..." kupitia mtandao wake wa Facebook.

Katika mahojiano ya Moja kwa moja na vituo tofauti vya radio Kaa La Moto alidai kuwa hawezi pandishwa studio moja na JOHNY SKANNY kwani yeye anajiamini anaweza bila mkono wa mtu naye JOHNY SKANNY kudai kuwa kama mziki umemshinda Kaa La Moto arudi bongo alipo kuwa maana yeye hachezi na watoto wa dogo kama KAA LA MOTO KIUMBE ndipo Kaa akaweza kutupia maneno makali facebook na kusema "Asiyehusika na HIPHOP....afanye nini?The Hiphop i do is Hardcore,and am proud my funs wame get use to it.I don't force commercial but nauza kama commercial.And about Freestyle,freestyle ni article kwa Hiphop.Na nukuu Solo Thang kwa nyimbo ya Mtazamo"Wanajiita ma emcee hawajui Mitindo Huru"..Let me remind ourselves the Element of HipHop..Mc,Rap,knowledge,Breakdance,Grafit,Dj.(from Brookyln)after that zikaongezeka zingine kama Freestyle,Beatboxing,Kitaaologia...nk.."

Hapo jana kupitia kipindi cha MWAKE MWAKE PILIPILIFM Chigulu na mzenzake Chriss walishindwa kuwatuliza wasanii hao hadi kupelekea kuwa wafanye kolabo wote wawili katika studio za SQ-RECORDS.

Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.  

NEW SONG ALERT: NYOTA NDOGO-SUBIRA YANGU| IPAKUE HAPA...

Hii ni ngoma mpya ya msanii wakike NYOTA NDOGO inayokwenda kwajina SUBIRA YANGU ambapo ngoma hii aliweza kuiachia hapo jana. Pata kuipakua hapa ivi upate ujumbe mtamu na Wakuelimisha.

NEW AUDIO | RABBIT KING KAKA FEAT RICH MAVOKO-NJOO | LISTEN AND DOWNLOAD HERE..

Hii ni nyimbo mpya kutoka KenyaTanzania ambapo ni moja ya Colabo iliyongojewa kwa muda mrefu,colabo hio inakwenda kwa jina la NJOO ambapo ni msanii wa Hip Hop ameshirikisha msanii wa Bongo flava kutoka Tanzania hapa nikiwa namzungumzia KING KAKA akiwa na RICH MAVOKO. Nyimbo hio imeachiliwa rasmi hii leo na wasanii hao wawili. pata kuiskiza na ku download hapa..