Hapo jana katika kituo cha radio cha Pwanifm Producer Tee kutoka TEE HITS aliweza kufunguka ya moyoni
Producer huyo aliweza kuulizwa anawaonaje hawa ma-manager wetu kutoka hapa Kenya na kuwa dai kuwa hakuna manager mzuri "Hawa manager wetu bado na sijapata kuona manager mzuri atakaye mmliki msanii wangu Dazlah ndio maana Candy and Candy walishindwa,mimi sitaki manager wakuwa atamfanyia video ya elfu ishirini alafu isemekane anammiliki Dazlah,ninachokitaka mimi ni manager wa kumfanyia Dazlah kama ni video ni Milioni kwenda mbele sio manager wa kumlipia Audio pekeake" Tee alisema.
Tee aliweza kuongeza kuwa hapa mkoani pwani msanii aliye juu wakwanza ni Dazlah wapili ni Sususmila na watatu Ally B,Tee aliweza kusawazisha fununu zilizokuwa zinaenea mtaani kuwa yeye alifunzwa kazi na Producer MOBIZ wa THURNDER SOUND alikanusha madai hayo na kudai kuwa yeye alienda THURNDER SOUND ki kazi sio kufundishwa alipoingia studio hizo yeye alikuwa ameiva tayari na alipotoka hapo ndipo akafungua studio yake na kuiita TEE HITS (TACH ZA MIBA).
Tee aliweza kuulizwa swali na Munga kuhusu msanii wakike aliyekuwa anammiliki kwa jina AZALIA na kudai kuwa wasanii wakike kutoka hapa mkoani ni changa moto lakini hakuzitaja changamoto hizo.
Comments
Post a Comment