DIAMOND PLATNUMZ AJIBU BARUA ALIYOANDIKIWA NA MSANII MEDA..PATA KUJUA ALICHOKISEMA DIAMOND KUHUSU MSANII HUYO
Hivi majuzi msanii kutoka Bongo/Tz anayefahamika kama MEDA ametunga wimbo wake akimuimbia msanii mkubwa Africa hit maker wa MY NUMBER ONE anayejulikana kama DIAMOND PLATNUMZ.
Meda
inasemekana kuwa anamkubali Diamond na kwamba huko kwao Iringa yeye ndio balozi
wa Diamond, alipitia tabu sana kumtafuta miaka miwili iliyopita na sasa
amefanya wimbo huu kama zawadi kwake na pia kuonyesha anavyo mkubali.
Wimbo wake huo uliojulika kama BARUA KWA DIAMOND aliweza kuuachia mapema wiki hii ambapo pia ukimtazama msanii MEDA vizuri anafanana na msanii huyo aliyeandikiwa barua yaani DIAMOND,mbinu za msanii huyo kumtafuta DIAMOND zilifua dafu pale NASSIB alikaa chini na kuuskiliza wimbo huo na ukamgusa kiasi cha kuwa hakuvumilia na kuingia katika mitandao yake na kumjibu msanii huyo baru yake.
Hapo jana kupitia mtandao wake wa Instagram DIAMOND alisema haya.
“Kiukweli simfahamu... Sijawai hata
kumuona, Wala kuzungumza nae.....na sio kwasababu Eti kaniimba mimi, hapana!...
ila ni userious na uzuri wa kazi aliyoifanya ndio vimenifanya nione ni vizuri
kumleta kwenu hapa wadau ili kwa pamoja tumsupport naye kesho na keshokutwa
afikie malengo ya kazi yake na kuwa Balozi mzuri wa nchi yetu kupitia Bongo
flavour..Huyu hapa! Anaitwa MEDA kutoka IRINGA” Hayo ndio aliyasema kupitia Instagram mapema jana.
Tizama video hio ya MEDA "BARUA KWA DIAMOND" hapa
Comments
Post a Comment