Wabunge wa hapanchini Kenya hii leo wamepigana ngumi, kun'gatana na kuoneshana ubabe zaidi bungeni kufuatia kutofautiana juu ya muswada tatanishi wa usalama
Wabunge wa upinzanzi walipinga muswada huo na kuanza kurusha karatasi sakafuni na kukatiza shughuli Bungeni humo
Mapendekezo ya muswada unaopingwa ni kwamba mshukiwa wa ugaidi anaweza kuzuiliwa kwa siku 360 kutoka siku 90 za awali huku uchunguzi ukiendelea.
Wabunge wa upinzani wanapinga muswada huo wenye utata kuhusu usalama maana wanasema unakiuka uhuru wa wakenya
Muswada huu umekuja baada ya kutokea mashambulizi yaliyofanywa na Al Shabaab wakitaka wanajeshi wa hapa nchini kuondoka Somalia.
Comments
Post a Comment