Skip to main content

#TGM_LYRICS: HII NI MISTARI YA NGOMA YA TOTTI AKIWA AMEMSHIRIKISHA CHIKUZEE "MIGOGORO"...

Hiki ni kitengo cha kuwa THEGREATMULLEY itakuwa inakupatia mistari ya kila ngoma kutoka kwa msanii wako unae mpenda kutoka Afrika Mashariki.

Leo tumeanza na ngoma inayozidi kutamba ndani ya anga za Afrika Mashariki amabayo inajulikana kama MIGOGORO kutoka kwa TOTTI MUSIC akiwa amempa shavu CHIKUZEE.

Chorus
Kila siku migogoro, migogoro, migogoro nawe
Kila kitu migogoro, migogoro, migogoro nawe
Mi staki migogoro, kila siku migogoro nawe
Mi Staki migogoro, kila kitu migogoro nawe

Verse 1
Wachonganishi hao, mpenzi wangu wee
Hawalali kukesha kusema unafiki hao, baby wangu wee
Usiskize maneno yao yana sumu hayo
Hawataki tupendane, wanataka tugombane
Hawataki niwe nawe, wanataka tuachane
Mara tumekosana nyumbani mara hatuongeleshani
Umenuna huongei, inaniuma sana
Umenuna huongei, inaniuma sanaaaaa

Chorus
Kila siku migogoro, migogoro, migogoro nawe
Kila kitu migogoro, migogoro, migogoro nawe
Mi staki migogoro, kila siku migogoro nawe
Mi Staki migogoro, kila kitu migogoro nawe

Verse 2
Visimu simu kila mara vyatugonganisha
Wanafiki hawachoki kutugombanisha
Kila siku ni unoko haya mambo gani
Hata tukifanya ya ndani mtachoka semeni
Wee ndio wangu unatambua
kila kukicha wanipa burudani
Wala Mimi siezi jua, kina fulani wanagere la nini
Mara nimechelewa nyumbani,mara eti niko na fulani
Umenuna huongei, inaniuma sana
Umenuna huongei, inaniuma sanaaa
Chorus
Kila siku migogoro, migogoro, migogoro nawe
Kila kitu migogoro, migogoro, migogoro nawe
Mi staki migogoro, kila siku migogoro nawe
Mi Staki migogoro, kila kitu migogoro nawe

Verse 3 (CHIKUZEE)
Nalipenda penzi lenu nikiwaona pamoja
Si kila siku vijimambo wengine vioja
Wanataka leta vijimambo kwenu nyie hamuelewi
Wanataka leta vijikesi kwenu nyie hamtambui
Oh wanoko hao, wanoko hao, wanoko hao wazome x2
Wazome wazome wazome wazome x2

Kama bado hujaweza kuupata wimbo huo upate hapa kwa ku download..

Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.  

NEW SONG ALERT: NYOTA NDOGO-SUBIRA YANGU| IPAKUE HAPA...

Hii ni ngoma mpya ya msanii wakike NYOTA NDOGO inayokwenda kwajina SUBIRA YANGU ambapo ngoma hii aliweza kuiachia hapo jana. Pata kuipakua hapa ivi upate ujumbe mtamu na Wakuelimisha.

NEW AUDIO | RABBIT KING KAKA FEAT RICH MAVOKO-NJOO | LISTEN AND DOWNLOAD HERE..

Hii ni nyimbo mpya kutoka KenyaTanzania ambapo ni moja ya Colabo iliyongojewa kwa muda mrefu,colabo hio inakwenda kwa jina la NJOO ambapo ni msanii wa Hip Hop ameshirikisha msanii wa Bongo flava kutoka Tanzania hapa nikiwa namzungumzia KING KAKA akiwa na RICH MAVOKO. Nyimbo hio imeachiliwa rasmi hii leo na wasanii hao wawili. pata kuiskiza na ku download hapa..