Skip to main content

EXCLUSIVE STORY| MANAGER WA WASOJALI BAND AONGELEA SWALA ZIMA LA WASANII WAKE KUTUMIA BEAT "HELLO" YA DIAMOND PLATNUMZ...




Ni wiki moja imepita tangu ngoma mpya ya WASOJALI BAND iliojulikana kama NITALIA NAWE kuachiliwa katika vituo vyote vya runinga/Radio humu nchini na kupokelewa vizuri na media zetu na baada ya hapo ngoma hio imezua mtafaruku baada ya watu mbali mbali ikiwemo washika dau pamoja na mashabiki kusema kwamba Beat iliotumika katika ngoma ile iliweza kuibwa kutoka kwa ngoma HELLO alioifanya star DIAMOND PLATNUMZ.

Manager wa vijana hawa wanaokuja kwa kasi zaidi anayetambulika kama ATHMAN BABA aliweza kulivalia njuga swala hilo na kuweka wazi,Akiongea na THE GREAT MULLEY kuhusu swala hilo BABA aliweza kusema kwamba wasanii wake hawajaiba beat yoyote bali ni yeye mwenyewe ndio aliweza kuiskiza nyimbo ile ya Diamond Platnumz na kuipenda zaidi na kutaka vijana wake wafanye kitu kama hicho ivyo basi ikamlazimu kuitafuta beat hio na kumpelekea Produza NOIZER na kumwambia asiweze kutoa ata kinanda ndani ya Beat ile na pia vijana wake wataweza kuimbia ndani ya mfumo ule ule Diamond aliyoimbia ndio pale wasanii wake wakaingia studio na kueka vocals katika beat ile "Kiukweli mimi ni mtu ninaye penda sana kusikiliza mziki mzuri ivyo basi niliupenda sana ule mziki alioutoa Diamond Platnumz uliojulikana kama "HELLO" ndio maana nilihangaika na kutafuta beat ile ili vijana wangu waeke mistari ndani ya beat hio bila kuguswa popote kwa hivyo me naeza sema sikuiba beat Ya Diamond nilipenda kazi yake ndio maana nikatamani kufanya kitu kama kile "Alisema hayo.


Pia aliweza kusema kwamba inahitajika tukuze mziki wetu ufike mbali sio kuukuza kwa kuukosoa yaani msanii akitoa nyimbo watu wanangojea kuskia hio nyimbo imeibwa wapi ama inatokana na nyimbo gani aliweza kulaani kitendo hicho na kusema kwamba tukiendelea ivyo mziki wetu utaishilizia hapa hapa Mariakani na hautaenda popote ivyo basi tupende mziki wetu ilitusongee mbele.


Pata Kuitazama video hio ya NITALIA NAWE hapa chini..

Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.  

NEW SONG ALERT: NYOTA NDOGO-SUBIRA YANGU| IPAKUE HAPA...

Hii ni ngoma mpya ya msanii wakike NYOTA NDOGO inayokwenda kwajina SUBIRA YANGU ambapo ngoma hii aliweza kuiachia hapo jana. Pata kuipakua hapa ivi upate ujumbe mtamu na Wakuelimisha.

NEW AUDIO | RABBIT KING KAKA FEAT RICH MAVOKO-NJOO | LISTEN AND DOWNLOAD HERE..

Hii ni nyimbo mpya kutoka KenyaTanzania ambapo ni moja ya Colabo iliyongojewa kwa muda mrefu,colabo hio inakwenda kwa jina la NJOO ambapo ni msanii wa Hip Hop ameshirikisha msanii wa Bongo flava kutoka Tanzania hapa nikiwa namzungumzia KING KAKA akiwa na RICH MAVOKO. Nyimbo hio imeachiliwa rasmi hii leo na wasanii hao wawili. pata kuiskiza na ku download hapa..