EXCLUSIVE VIDEO| KILE KICHUPA K ILICHOKUWA KINANGOJEWA KUTOKA KWA WASOJALI BAND WAKIWA NA KELECHI NDIO HICHI HAPA "NITALIA NAWE"
Baada ya vijana hawa kuzana kidogo chini ya maji,wameibuka na hii video inayojulikana kama NITALIA NAWE.
Katika mtazamo wetu, katika video zao zote hii ndio imetoka tofauti kabisa na vile mashabiki walivyokuwa wanatarajia ambapo kuna shots kali kali ndani ya kichupa hiki,Video hii bado iko chini ya uongozi wa RICKY BEKKO ambaye ndio director anayeongoza video zote za WASOJALI BAND kuanzia pale walipoingia katika kinyang'anyiro hichi cha mziki.
Katika video hii na nyimbo hii ilioketiwa chini na Produza NOIZER kutoka GREEN HOUSE kumeonekana msanii mpya ambaye anakwenda kwa jina la KELECHI AFRICANA ambaye kwasasa tetesi zina sema huyo ni mmoja ya msanii ambaye yuko chini ya uongozi wa ATHMAN BABA chini ya lebo ya KUBWA ENT.
Pata kuitazama video hio hapa chini...
Comments
Post a Comment