NEW VIDEO ALERT| EDDY TICHA ADAI KWAMBA AMECHOKA KUSKIKA SAUTI,TAZAMA "ZAWADI" VIDEO YAKE MPYA
Baada ya kuwaporomoshea mashabiki zake nyimbo album mzima bila video hapo mwaka jana msanii aliyetimia vocals na uandishi EDDY TICHA amejitokeza katika kioo chako.
Wimbo huu unakwenda kwa jina ZAWADI ambapo video imeweza kuandaliwa na LYNKE JR kutoka kampuni ya DA MUSIK LAB na audio yake kuketiwa chini na produza Morbiz (Sheriff) ndani ya studio za THURNDER SOUND.
Katika miaka yote mwaka wa 2018 unaonekana ndio mwaka ambao mkali wa masauti Shembwana Masauti ameweza kufanya kazi nyingi nzuri na za ghali sana. Mkali wa 'vocals' Masauti mwaka jana aliweza kudondosha ngoma kali takriban kama nne kwa mfululizo amabazo ziliweza sana na kwasasa kibao kinachotatiza anga kinaitwa KIBOKO ambacho kibao icho kinaendelea kufanya vizuri ndani Afrika Mashariki. Hapo jana Presenter mkubwa kutoka MileleFmJalang'o almaarufu kama Mzee Jalas Mwenyewe aliweza kusema msanii huyu huu mwaka ndiye atakaye sumbua kulingana na usimamizi wake mzuri pamoja na kazi zake zinazoweza kupita kiwango. Hii Hapa ndio kazi yake MAsauti mpya inayokwenda kwajina KIBOKO
Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.
Comments
Post a Comment