Skip to main content

HAYA NDIO ALIYOYASEMA MKONGWE WA MUZIKI WA AFRIKA MASHARIKI SAIDA KAROLI BAADA YA DIAMOND NA RAYVANY KUIPIGA TENA SALOME...Soma hapa zaidi

Msanii wa nyimbo za asili Saida Karoli aliyevuma kitambo, amefunguka na kusema kuwa kitendo cha msanii Diamond Platnum kurudia moja ya kazi yake anajihisi kuzaliwa upya.


Saida Karoli ambaye aliwahi kufanya vizuri na nyimbo kama 'Mapenzi kizunguzungu', Kaisiki, Maria Salome na nyingine kibao na alifanikiwa kuliteka soko la Afrika Mashariki kwa nyimbo hizo na kujipatia umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Saida Karoli amesikika kwenye moja ya clip ambayo ameiposti Diamond Platnumz kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mwanzoni waandishi wa habari walisha msahau walikuwa hawamtafuti tena, lakini hata baadhi ya watu pamoja na ndugu zake walikuwa wakiambiwa kuwa amekufa lakini baada ya kazi ya Diamond Platnumz kutoka imerejesha watu kwenye himaya yake kwani wameanza kumtafuta na kumpigia simu sana.
"Mimi nimejisikia vizuri maana hii kazi tunayofanya ni kwa ajili ya mashabiki, mashabiki ndiyo wadau wetu wanaotufanya sisi tuwe juu kwa hiyo si kazi ya kwangu mimi peke yangu, ila mimi kama mimi nimejisikia vizuri kusikiliza kwa sababu hata vyombo vya habari vilinisahau leo hii vinanitafuta, haya ndugu zangu baadhi na wengine wanajua hata siko duniani wanajua nilishakufa lakini leo hii naona watu mbalimbali wananitafuta kweli nimefunguka najihisi kuzaliwa upya" alisikika Saida Karoli.

Hii Hapa ndio video hio kutoka kwa uongozi wa WCB Wasafi inayokwenda kwajina SALOME

Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.  

NEW SONG ALERT: NYOTA NDOGO-SUBIRA YANGU| IPAKUE HAPA...

Hii ni ngoma mpya ya msanii wakike NYOTA NDOGO inayokwenda kwajina SUBIRA YANGU ambapo ngoma hii aliweza kuiachia hapo jana. Pata kuipakua hapa ivi upate ujumbe mtamu na Wakuelimisha.

NEW AUDIO | RABBIT KING KAKA FEAT RICH MAVOKO-NJOO | LISTEN AND DOWNLOAD HERE..

Hii ni nyimbo mpya kutoka KenyaTanzania ambapo ni moja ya Colabo iliyongojewa kwa muda mrefu,colabo hio inakwenda kwa jina la NJOO ambapo ni msanii wa Hip Hop ameshirikisha msanii wa Bongo flava kutoka Tanzania hapa nikiwa namzungumzia KING KAKA akiwa na RICH MAVOKO. Nyimbo hio imeachiliwa rasmi hii leo na wasanii hao wawili. pata kuiskiza na ku download hapa..