EXCLUSIVE STORY||| HIKI NDIO KIWANGO CHA HELA MADAM BOSS AKOTHEE ANALIPISHA UKITAKA COLLABO NAYE WAAAAH!! JIPANGE MTU WANGU .....
Kwa mujibu wa Citizen, taarifa hii ikufikie kama ni msanii na unahitaji kufanya collabo na Akothee basi unatakiwa kuandaa mfuko wako kisawasawa. Akothee ametangaza kiwango cha Pesa ambacho utatakiwa kumlipa ili uweze kuingia naye studio kuwa ni Shilingi Milioni 1 za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi Milioni 21 za Tanzania.
“Ukiwa msanii, hautakiwi kukimbilia kusaini deal za record labels, uanweza kutengeneza pesa zako kuoitia social media. Usijikalishe na kusubiri pesa zije. Sasa kwa upande wangu wala usijisumbue kunipigia simu kama hauna shilingi Milioni 1 za kufanya collabo,” – Akothee
Akothee amesema anatafikiria kusaini deal na lebel za Marekani endapo tu zitakuwa na maslahi ya kueleweka.

Star huyo wa single ya ‘Yuko Moyoni’ hivi karibuni amefanikiwa kushinda tuzo mbili za best East African female artist zilizotolewa na waandaaji wa jarida la African Muzik Magazine (AFRIMMA) pamoja na African Entertainment Awards USA (AEAUSA).
Comments
Post a Comment