Skip to main content

EXCLUSIVE STORY|||JE AZMA YA YA NASSIZU MURUME KWENDA WCB BADO IKO? PATA STORY NZIMA HAPA

Nassizu ni msanii kutoka Meru/Kenya mwenye asili ya kipwani ambapo ni mmoja ya wasanii waliojaliwa na vocals na anapiga sana mtindo wa afro pop.
Mapema mwaka huu Nassizu aliweza kuweka wazi kwamba yuko tayari kuhamia TZA na kujiunga na team nzima ya WCB na kuonekana amepiga picha ndani ya studio izo za WASAFI akiwa na muanzilishi wa Record lable hio hapa namzungumzia DIAMOND PLATNUMZ ambapo mitandao yote iliweza kuwataarifu mashabiki anahamia pande zile za +255.

Nassizu ambaye kwasasa anatamba na nyimbo yake inayokwenda kwajina MAWAZO tuliweza kuwasiliana naye na kuweza kutudokezea kwamba azma yake kwenda W.C.B bado iko tena sana ila kuna vitu kadhaa ambayo management yake inayokwenda kwajina WATANASHATI CLASSIC bado inavishughulikia ndio akanyage kule akiwa kikamilifu "Si unajua lazima ujifue vizuri ndio uwende kule mpaka uwe na mikoba ya kueleweka maana nikienda WCB siendi kama Nassizu ila naenda kama Kenya" Tuliweza kumnukuu akiyasema hayo na kuongezea kwamba mwaka ujao Mungu akimuwezesha ataweza kufika uko uko.


Pata kuitazama video yake mpya ya MAWAZO iliyoongozwa na JOHNSON KYALO "MAWAZO"

Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE HII HAPA : MASAUTI KATABIRIWA KUWA "THE NEXT BIG THING" NDANI YA MWAKA 2019 JE UNAJUA NI NANI ALIYEMTABIRIA?..Soma hapa

Katika miaka yote mwaka wa 2018 unaonekana ndio mwaka ambao mkali wa masauti Shembwana Masauti ameweza kufanya kazi nyingi nzuri na za ghali sana. Mkali wa 'vocals' Masauti mwaka jana aliweza kudondosha ngoma kali takriban kama nne kwa mfululizo amabazo ziliweza sana na kwasasa kibao kinachotatiza anga kinaitwa KIBOKO ambacho kibao icho kinaendelea kufanya vizuri ndani Afrika Mashariki. Hapo jana Presenter mkubwa kutoka MileleFmJalang'o almaarufu kama Mzee Jalas Mwenyewe aliweza  kusema msanii huyu huu mwaka ndiye atakaye sumbua kulingana na usimamizi wake mzuri pamoja na kazi zake zinazoweza kupita kiwango. Hii Hapa ndio kazi yake MAsauti mpya inayokwenda kwajina KIBOKO

EXCLUSIVE: DOWNLOAD WIMBO MPYA WA TANZANITE ALIYO MUIMBIA LULU WA BONGO MOVIE

Pata kudownload na kuskiza hapa chini....

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.