Skip to main content

ZIKKY KENYA ARUSHA DONGO KWA MA-"PRESENTER" NA "PROMOTER" WANAOBABAIKIA WASANII WA NJE.....

Ziky Kenya ni mmoja ya wasanii wazuri tu kutokea hapa nchini Kenya katika jimbo la Mombasa na yuko chini ya Madam boss Akothee.
Msanii huyo mapema hii leo ameweza kuweka wazi jambo linalo mkera na kumkereketa kuhusiana na mziki wa Mombasa na Kenya kwa ujumla.Ziky aliweza kunyoosha maneno yake yakiwa yamejawa na uchungu mwingi kutoka roho ambapo aliweza kueleza bila kuogopa jinsi washikadau wetu wamuziki wanababaikia wasanii kutoka nchi za nje wakiwa wanakuja kufanya matamasha yao mjini Mombasa.

Ziky ambaye yuko chini ya uongozi wa AKOTHEE SAFARIS mapema Ijumaa tarehe mbili mwezi wakumi na moja saa tano na takriban dakika arubaini aliweza kuyamwaga maneno haya "HIVI HUYU DOGO NDO NANI ?? NAONA AMEPEWA BONGE MOJA LA SUPPORT MOMBASA ZAIDI HATA YA WASANII WA HAPA .WENGINE JUZI WALIACHA HATA MAKAZI YAO KWA KUZUNGUKA BARABARANI NA KUKODISHA MAGARI ILI IONEKANE JAMAA ANAMASHABIKI ... MBONA MKIWAPA SHOW WAKINA Susumila Yusuf Chikuku Chikuzee FRANK DEE NYOTA NDOGO Kaa La Moto Kiumbe MSIENDE KUZUNGUKA MITAANI NA MAGARI KUTANGAZA SHOW?? SOKO LETU HILO SIJUI NDO TUITE UBABAIKAJI AMA NINI .TENA HAO HAO MNAOWABABAIKIA HATA WAKICHUKUA PICHA NA NYINYI KIBARUA BADO UNACHO WEWE JUU YEYE HANA MUDA WA KUKUPOST. .TUKOMAENI NA TUPENDE VYETU TUBABAIKIE VYETU TUONE KAMA KINA KELECHI MASAUTI Wynas WillyNA WENGINEHAWATA BABAIKIWA NNJE .. HII NAIONA HAPA MOMBASA NAIROBI HAKUNA MAMBO HAYA VIJANA WANA NG'ANG'ANA KUEKEZA KWA MZIKI WASIMAMIZI NAO WANA NG'ANG'ANA KUTOA SHOW NA KUBABAIKIA WASANII WA NNJE ... HIVI MNATAKA WATU WAIMBE VIPI NA WATOE VIDEO ZA VIPI NDO HIZO SHOW MNAZOPEANA WASANII WA NNJE MUWAPE WASANII WA NYUMBANI? SAWA HATUKUSOMA HAO MNAOWALETA NDO WASOMI????" Uku akiwa amefuatiliza na screenshot promota Rozay akiwa amempost msanii Enock Bella kutoka kundi vunjika la Yamoto Band.


Comments

Popular posts from this blog

EXCLUSIVE HII HAPA : MASAUTI KATABIRIWA KUWA "THE NEXT BIG THING" NDANI YA MWAKA 2019 JE UNAJUA NI NANI ALIYEMTABIRIA?..Soma hapa

Katika miaka yote mwaka wa 2018 unaonekana ndio mwaka ambao mkali wa masauti Shembwana Masauti ameweza kufanya kazi nyingi nzuri na za ghali sana. Mkali wa 'vocals' Masauti mwaka jana aliweza kudondosha ngoma kali takriban kama nne kwa mfululizo amabazo ziliweza sana na kwasasa kibao kinachotatiza anga kinaitwa KIBOKO ambacho kibao icho kinaendelea kufanya vizuri ndani Afrika Mashariki. Hapo jana Presenter mkubwa kutoka MileleFmJalang'o almaarufu kama Mzee Jalas Mwenyewe aliweza  kusema msanii huyu huu mwaka ndiye atakaye sumbua kulingana na usimamizi wake mzuri pamoja na kazi zake zinazoweza kupita kiwango. Hii Hapa ndio kazi yake MAsauti mpya inayokwenda kwajina KIBOKO

EXCLUSIVE: DOWNLOAD WIMBO MPYA WA TANZANITE ALIYO MUIMBIA LULU WA BONGO MOVIE

Pata kudownload na kuskiza hapa chini....

EXCLUSIVE AUDIO| CHIKUZEE-KUNGURU MWEUSI|LISTEN AND DOWNLOAD HERE

Baada ya kimya cha muda msanii na mkali wa vocals kutoka hapa Kenya CHIKUZEE ameachia mzigo mpya kutoka NUMBER RECORDS unajulikana kama KUNGURU MWEUSI. Ujio huu wa Chikuzee umekaa tofauti kabisa na alivyozoeleka na mitindo yake ya hapo awali,round hii ameamua kuingia katika mtindo wa TAARAB na ili kuonesha ujuzi wake na mashairi yake yalivyokomaa. Pata kuudownload KUNGURU MWEUSI hapa.. BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD KUNGURU MWEUSI.